Search this website | ||||
Ujumbe, 2 Machi 2018 - Tokeo la MirjanaOther languages: English, العربية, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Magyar, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Shqip, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt, Українська
“Wanangu wapendwa, Baba wa Mbinguni amenifanyia makuu, jinsi anavyowafanyia wale wote wanaompenda sana na kwa wema na uaminifu na wanaomtumikia kwa ibada. Wanangu, Baba wa Mbinguni anawapenda na kwa ajili ya upendo wake mimi nipo hapa pamoja nanyi. Ninasema nanyi: kwa nini hamtaki kuona ishara? Pamoja naye yote ni rahisi zaidi: hata mateso, tunayoishi pamoja naye, ni mepesi zaidi, maana kuna imani. Imani husaidia mateso, na maumivu pasipo imani huongoza katika kukata tamaa. Mateso tunayoyaishi na kuyatolea kwa Mungu, huinua mtu. Je, Mwanangu hakuukomboa ulimwengu kwa njia ya mateso yake makali? Mimi, kama mama yake, katika maumivu na mateso nilikaa pamoja naye, kama vile ninavyokaa pamoja nanyi. Wanangu, mimi nipo pamoja nanyi katika maisha: katika maumivu na mateso, katika furaha na upendo. Kwa hiyo muwe na matumaini: matumaini ndiyo yanayotuwezesha kuelewa ya kuwa hapa, kwenye mateso, ni uhai. Wanangu, mimi nasema nanyi; sauti yangu inasema na nafsi yenu, Moyo wangu unasema na moyo wenu: Enyi, mitume wa upendo wangu, Moyo wangu wa kimama jinsi gani unavyowapenda. Mambo haya nataka kuwafundisha. Jinsi gani Moyo wangu unataka muwe wakamilifu, lakini mtakuwa hivyo tu wakati nafsi, mwili na upendo yatakapoungana ndani yenu. Kama wanangu nawaombeni: salini sana kwa ajili ya Kanisa na kwa wahudumu wake, kwa wachungaji wenu, ili Kanisa liwe kama Mwanangu anavyolitaka: safi kama maji ya chemchemi na limejaa upendo. Nawashukuru. ” To compare Medjugorje messages with another language versions choose | | |||
Our Lady of Medjugorje Messages Find messages Enter words or phrase Random Messages “Pray, and in prayer you are open to God's will; in this way, in everything you do, you realize God's plan in you and through you.” ( From message, 25 Machi 2003 ) | Medjugorje Live Current time in Medjugorje (CET): Deep concern & disturbing information: Latest news & articles 15 Aprili 2017 24 Septemba 2016 5 Aprili 2016 2 Oktoba 2015 Latest videos 11 Juni 2018 10 Mei 2018 13 Aprili 2018 31 Machi 2018 16 Machi 2018 Most read articles Most watched videos Most watched Medjugorje Photos Gallery albums Favorite content related to Medjugorje" | |||
Our Lady of Medjugorje Messages Medjugorje Videos Medjugorje News & Articles Medjugorje Web Sites Links Picture & Photo Galleries The Polls | Copyright © 2005-2024 Medjugorje WebSite medjugorje.ws medjugorie.ws medugorje.ws ourlady.eu and content contributors | |||