Search this website | ||||
Ujumbe, 2 Septemba 2016 - Tokeo la MirjanaOther languages: English, العربية, Беларуская, Čeština, Deutsch, Español, Français, Hrvatski, Italiano, Kiswahili, Latviešu, Nederlands, Polski, Português, Română, Русский, Slovenčina, Slovenščina, Suomi, Tiếng Việt
“Wanangu wapendwa, kulingana na mapenzi ya Mwanangu na upendo wangu wa kimama naja kwenu, wanangu, hasa kwa wale ambao hawajajua bado upendo wa Mwanangu. Ninakuja kwenu mnaonifikiria, mnaoomba msaada wangu. Ninawapa upendo wangu wa kimama na kuwaletea baraka ya Mwanangu. Mnayo mioyo safi na wazi? Mnaona dalili za uwepo wangu na upendo wangu? Wanangu, katika maisha yenu ya dunia igieni moyo na mfano wangu. Maisha yangu yalikuwa maumivu, ukimya, imani na matumaini pasipo mipaka katika Baba wa Mbinguni. Hakuna kitu cha bahati: si maumivu, si furaha, si mateso, si upendo. Hizo zote ni neema ambazo Mwanangu anawapeni na zinazowaongoza kwenye uzima wa milele. Mwanangu anawaomba mapendo na sala ndani yake. Kupenda na kusali ndani yake maana yake — kama Mama nataka kuwafundisha — ni kusali katika ukimya wa nafsi zenu, si kusema kwa midomo tu. Ni tendo dogo zuri litendwalo kwa jina la Mwanangu; ni uvumilivu, rehema, upokeaji wa maumivu na kujitolea kwa ajili ya wengine. Wanangu, Mwanangu huwatazama. Ombeni ili ninyi pia muuone uso wake, na ili uso huo uweze kufunuliwa kwenu. Wanangu, mimi nawafunulia ukweli halisi wa pekee. Salini kwa kuyaelewa na kuweza kueneza mapendo na matumaini, kwa kuweza kuwa mitume wa upendo wangu. Moyo wangu wa kimama hupenda hasa wachungaji. Iombeeni mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru. ” To compare Medjugorje messages with another language versions choose | | |||
Our Lady of Medjugorje Messages Find messages Enter words or phrase Random Messages “Pray, little children, in a special way for all those who have not come to know God's love. Pray that their hearts may open and draw closer to my heart and the Heart of my Son Jesus, so that we can transform them into people of peace and love.” ( From message, 25 Januari 2004 ) | Medjugorje Live Current time in Medjugorje (CET): Deep concern & disturbing information: Latest news & articles 15 Aprili 2017 24 Septemba 2016 5 Aprili 2016 2 Oktoba 2015 Latest videos 11 Juni 2018 10 Mei 2018 13 Aprili 2018 31 Machi 2018 16 Machi 2018 Most read articles Most watched videos Most watched Medjugorje Photos Gallery albums Favorite content related to Medjugorje" | |||
Our Lady of Medjugorje Messages Medjugorje Videos Medjugorje News & Articles Medjugorje Web Sites Links Picture & Photo Galleries The Polls | Copyright © 2005-2024 Medjugorje WebSite medjugorje.ws medjugorie.ws medugorje.ws ourlady.eu and content contributors | |||