Web address of the page: https://www.medjugorje.ws/sw/messages/highlight?find=wetu 
www.medjugorje.ws » Our Lady of Medjugorje Messages » Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wetu'

Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wetu'

Wanangu wapendwa! Nipo pamoja nanyi kuwaambia kuwa nawapenda na ninawasihi sana muombe maana shetani ana nguvu na kila siku nguvu zake zinazidi kuimarika kupitia wale waliochagua kifo na chuki. Ninyi, wanangu, muwe maombi na mikono yangu ya upendo iwanyooshee wote walio gizani na kuitafuta nuru ya Mungu wetu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.