Our Lady of Medjugorje Messages containing 'ya'
Total found:
198
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga
ya
joto la jua. Huo ni wakati wa neema ambao Mungu anawajalia kwa njia
ya
uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa uongofu binafsi na kwenye sala katika familia zenu. Maandiko matakatifu yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu
ya
kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalikeni tena kupenda na kutohukumu. Mwanangu, kwa mapenzi
ya
Baba aliye mbinguni, alikuwapo pamoja nanyi ili awaonyesheni njia
ya
wokovu, awaokoeni si awahukumuni. Na ikiwa mnataka kumfuata Mwanangu, msihukumu na mpende, kama vile Baba aliye mbinguni anavyowapenda ninyi. Hata wakati mnapoteseka sana, au mnapojikwaa chini
ya
msalaba, msikate tamaa, msihukumu, bali kumbukeni kwamba mnapendwa, na msifuni Baba aliye mbinguni kwa upendo wake. Wanangu, msiiache njia ninayowaongozeni. Msikimbie kwenye maangamizi. Kusali na kufunga itawapa nguvu zaidi ili mweze kuishi kama vile baba wa Mbinguni atakavyo; ili muwe mitume wangu wa imani na upendo; ili maisha yenu iwe na baraka
ya
wale mnaowaona; ili muwe kitu kimoja na baba aliye mbinguni na Mwanangu. Wanangu, huu ni ukweli wa pekee, ukweli uletao wongofu wenu na kisha wongofu wa wengine wote wasiojua maana
ya
neno kupenda. Wanangu, Mwanangu aliwapeni wachungaji: muwalinde, na muwaombee. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Mei 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni kuwa na nguvu na imara katika imani na katika sala, ili sala zenu ziwe zenye nguvu za kuweza hata kufungua moyo wa Mwanangu mpendwa Yesu. Salini enyi wanangu wadogo, bila kukoma, ili moyo wenu ujifungue kwa upendo wa Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi, nawaombea ninyi nyote nikasali kwa ajili
ya
uwongofu wenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, katika wakati huu wa wasiwasi nawaalikeni tena kutembea nyuma
ya
Mwanangu, na kumfuata. Nayajua maumivu, mateso na taabu zenu, lakini katika Mwanangu mtapumzika, ndani yake mtapata amani na wokovu. Wanangu, msisahau
ya
kuwa Mwanangu amewakomboa ninyi kwa msalaba wake akawajalieni kuwa tena wana wa Mungu na kuwafundisha kumwita tena "Baba" yenu, Mungu aliye mbinguni. Ili muwe wapenzi wa Mungu Baba, basi muwe na mapendo na msamaha, kwa kuwa Baba yenu ni upendo na msamaha. Salini na fungeni, kwa maana hii ndiyo njia
ya
kujua na kumfahamu Baba aliye mbinguni. Mtakapomjua huyo Baba, mtafahamu
ya
kuwa Yeye tu ni muhimu kwenu (Maria Mtakatifu amenena hayo kwa nguvu na amkazo sana). Mimi, nikiwa Mama, nataka wanangu wawe watu wenye umoja ambamo Neno la Mungu husikilizwa na kutekelezwa. Kwa hiyo, enyi wanangu, mfuateni Mwanangu, muwe kitu kimoja naye, muwe wana wa Mungu. Pendeni wachungaji wenu kama vile Mwanangu alivyowapenda alipowaita kuwatumikia ninyi. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 2 Julai 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama nawaomba mnipe mioyo yenu ili niweze kumtolea Mwanangu, ili naye aweze kuiokoa, kuiokoa kutoka uovu wote unaowafanya daima kuwa watumwa na unaowafanya kuwa mbali na ule Wema wa pekee, yaani Mtoto wangu, anayewaokoa kutoka yote yale yanayowaongoza kwenye njia
ya
uovu na kuwaondolea amani. Mimi natamani kuwaongoza kwenye uhuru wa ahadi za Mtoto wangu, kwa kuwa natamani hapa yatimizwe hasa hasa mapenzi
ya
Mungu, ili kwa kupatanishwa na Baba wa Mbinguni, kufunga na kusali, waweze kuzaliwa mitume wa mapendo
ya
Mungu, yaani mitume watakaoeneza kwa mapendo na uhuru, Mapendo
ya
Mungu kwa watoto wangu wote, mitume watakaoeneza mapendo aminifu kwa Baba wa Mbinguni na hivyo kufungua milango
ya
mbingu. Watoto wapenzi, toeni furaha
ya
mapendo yenu na mshikamano wenu kwa wachungaji wenu kama vile Mtoto wangu alivyowaomba wao kutoa furaha hiyo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, tafadhali muelewe, muwe tayari wote, kwa matumaini makuu, kufungua mioyo yenu; hivyo mngeelewa yote, mngeelewa kwa upendo gani nawaiteni, kwa upendo gani nataka kuwageuza, ili kuwafurahisha, kwa upendo gani nataka kuwafanya wafuasi wa Mwanangu na kuwapa amani katika ukamilifu wa Mwanangu. Mngeelewa ukuu wa moyo wangu wa kimama, kwa hiyo, wanangu, salini, maana kwa njia
ya
kusali tu imani yenu hukua na upendo wenu huzaliwa, upendo ambao utapunguza uzito wa msalaba kwa maana hamtakuwa peke yenu kuubeba. Katika umoja na Mwanangu, tukuzeni jina la Baba wa Mbinguni. Salini, salini mpate tuzo la upendo, maana upendo ni ukweli wa pekee, upendo husamehe yote, hutumikia wote na kuwaona wote kama ndugu. Enyi wanangu, mitume wangu, udhamini ambao Baba wa Mbinguni amewawekeni, kwa njia yangu, mtumishi Wake, ni kitu kikubwa, ili kusaidia wale wasiomjua, kusudi zapatanishwe naye, kusudi wamfuate, kwa hiyo nawafundisheni kupenda, maana mkiwa na upendo tu mnaweza kumjibu. Nawaalikeni tena: pendeni wachungaji wenu, salini ili katika wakati huu wa shida jina la Mwanangu atukuzwe kwa njia
ya
mwongozo wao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo pia Yeye Aliye Juu anijalia neema
ya
kuwa pamoja nanyi na kuwaongoza mpate kutubu. Siku hata siku Mimi napanda mbegu na kuwaalika kutubu ili muweze kuwa sala, amani, upendo na ngano ambayo ikifa huzaa mara mia. Sipendi, wanangu wapendwa, mpate kujuta kwa yote mliyoweza kufanya wala hamkufanya. Kwa hiyo, enyi wanangu, tena kwa moyo wa furaha semeni: “ Nataka kuwa ishara kwa watu wengine”. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawapendeni, ninyi nyote, watoto wangu nyote, muwe wote moyoni mwangu, ninyi nyote mmepata upendo wangu wa kimama na ninatamani kuwaongoza nyote ili mjue furaha
ya
Mungu. Kwa hiyo nawaalikeni: nahitaji mitume wanyenyekevu ambao, kwa moyo mkunjufu, wanapokea Neno la Mungu na ambao wako tayari kuwasaidia watu wengine ili, kwa njia
ya
Neno la Mungu, waelewe maana
ya
maisha yao. Ili muweze kufanya hayo, wanangu, yawapasa, kwa njia
ya
kusali na kufunga, kusikiliza kwa moyo mkunjufu na kujifunza kujidhili au kujinyenyekesha. Yawapasa kujifunza kukataa yote yanayowatenganisha na Neno la Mungu na kutamani tu yanayowakaribisha. Msiogope, mimi nipo hapa. Ninyi si peke yenu. Namwomba Roho Mtakatifu ili awafanye wapya, ili awaimarishe. Namwomba Roho Mtakatifu, ili mkisaidia wengine, muweze kujiponya nyinyi wenyewe. Naomba ili, kwa njia yake, muwe wana wa Mungu na mitume wangu.
”
Kisha kwa mahangaiko makubwa Bikira Maria alisema:
“
K
wa ajili
ya
Yesu, kwa ajili
ya
mwanangu, pendeni wale ambao Yeye aliwaita mkitamani baraka
ya
mikono ile ambayo Yeye tu ameyaweka wakfu. Msiyaruhusu maovu yatawale. Nawaalikeni tena: ni kwa njia
ya
wachungaji wangu tu moyo wangu utashinda. Msiyaruhusu maovu yawatenganisheni na wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa! nawapendeni kwa upendo wa kimama, na kwa subira
ya
kimama nangojea upendo wenu na ushirikiano wenu. Nasali ili muwe jumuiya
ya
wana wa Mungu na wanangu. Nasali ili muweze kuwa jumuiya inayojihuisha kwa furaha na imani na upendo wa Mwanangu. Wanangu, nawakusanya kama mitume wangu na nitawafundisha jinsi
ya
kuwajulisha wengine upendo wa Mwanangu, na jinsi
ya
kuwafikishia habari njema, ambaye ni Mwanangu. Nipeni mioyo yenu iliyo wazi na iliyosafishwa, nami nitaijaza upendo wa Mwanangu. Upendo wake utaipa maisha yenu maana nami nitatembea pamoja nanyi. Nitakuwa pamoja nanyi hata tumfikie Baba wa Mbinguni. Wanangu, wataokoka tu wale ambao watatembea kwa upendo na imani kumwelekea Baba wa Mbinguni. Msiogope, nipo pamoja nanyi! Muwaamini wachungaji wenu kama Mwanangu alivyowaamini wakati alipowachagua, na muwaombee ili waweze kupata nguvu na upendo wa kuwaongozeni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni mjifungulie kwa sali. Sala itasababisha miujiza ndani yenu na kwa njia yenu. Kwa hiyo, enyi wanangu, kwa moyo mkunjufu mtafuteni Yeye Aliye Juu ili awapeni nguvu
ya
kuwa wana wa Mungu, na yule Shetani asiwatikiseni kama matawi yatikiswavyo na upepo. Kateni shauri tena, wanangu, kwa Mungu na tafuteni tu mapenzi yake, hapo mtapata furaha na amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa moyo wa kimama nawaalikeni tena kupenda, kusali bila kukata tamaa kwa zawadi
ya
upendo, kumpenda Baba wa Mbinguni zaidi
ya
yote. Mtakapompenda Yeye, mtajipenda wenyewe na jirani zenu. Mambo hayo hayawezi kutengana. Baba wa Mbinguni yumo katika kila mtu, hupenda kila mtu na kumwita kila mtu kwa jina lake. Kwa hiyo, wanangu, kwa njia
ya
kusali sikilizeni atakalo Baba wa Mbinguni. Ongeeni na Yeye. Muwe na uhusiano wa binafsi pamoja na Baba, atakayeufanya mkubwa zaidi uhusiano wake nanyi, jumuhiya
ya
wanangu, mitume wangu. Kama Mama napenda kwamba, kwa njia
ya
upendo kumwelekea Baba wa Mbinguni, inukeni juu
ya
ubatili wa malimwengu na muwasaidie wengine kujua na kumjongea polepole Baba wa Mbinguni. Wanangu, salini, salini, salini kwa zawadi
ya
upendo, kwa sababu upendo ndiye Mwanangu. Muwaombee wachungaji wenu, ili wawapende ninyi siku zote, kama vile Mwanangu alivyowapenda ninyi na kuonyesha akitoa maisha yake kwa wokovu wenu. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni nyote kusali. Fungueni kwa kina mlango wa mioyo yenu, enyi wanangu, kwa sala, sala
ya
moyo na hivyo Yeye Aliye Juu ataweza kufanya kazi katika uhuru wenu na kuanzisha uongofu wenu. Hivyo imani yenu itakuwa imara kiasi cha kuweza kusema kwa moyo wenu wote: "Mungu wangu na yote yangu". Halafu mtaweza kuelewa, wanangu,
ya
kuwa duniani hapa yote hupita. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo wa kimama na uvumilivu wa kimama naona kutangatanga kwenu na kuendelea kupotea kwenu. Kwa sababu hiyo mimi nipo pamoja nanyi. Nataka kwanza kabisa kuwasaidieni kupata kujijua ninyi wenyewe, ili baadaye muweze kuelewa na kutambua yote yanayowazuia kujua bila unafiki na kwa moyo wote upendo wa Baba wa Mbinguni. Wanangu, Baba hujulikana kwa njia
ya
msalaba: kwa hiyo msikatae msalaba: kwa msaada wangu, mkafanye bidii kuuelewa na kuupokea. Mtakapoweza kuupokea msalaba, mtaelewa pia upendo wa Baba wa Mbinguni. Mtatembea pamoja na Mwanangu na mimi. Mtajipambanua na wale ambao hawakujua upendo wa Baba wa Mbinguni, kujitofautisha na wale wanaomsikiliza lakini hawamwelewi, na wale wasioenda pamoja naye, na wasiomjua. Mimi nataka ninyi mjue ukweli wa Mwanangu na muwe mitume wangu; ili, kama wana wa Mungu, muwe na mawazo yaliyo juu
ya
mawazo
ya
kibinadamu na siku zote na katika yote mkatafute kila mara mawazo
ya
Mungu. Wanangu, salini na fungeni ili muweze kuelewa yote ninayowaombeni. Muombee wachungaji wenu mkatamani kujua, mkishirikiana nao, upendo wa Baba wa Mbinguni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mfalme wa amani ili Yeye awapatie amani Yake. Ninyi, wanangu, salini, salini, salini. Matunda
ya
sala yatajionyesha kwenye nyuso za watu waliojitoa kwa Mungu na Ufalme wake. Mimi pamoja na mwanangu Yesu tunawabariki nyote kwa baraka
ya
amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Ili mpate kuwa mitume wangu na kuweza kusaidia wale walioko katika giza, ili waweze kuujua mwanga wa upendo wa Mwanangu, mnapaswa kuwa na moyo safi na mnyenyekevu. Hamwezi kusaidia ili Mwanangu azaliwe na kutawala mioyoni mwa wale wasiomjua, iwapo Yeye hatawali moyoni mwenu. Mimi nipo pamoja nanyi, natembea pamoja nanyi kama mama, nabisha hodi katika moyo wenu, usioweza kufunguka bila
ya
kuwa mnyenyekevu. Mimi nasali, lakini salini nanyi pia, wanangu wapendwa, ili muweze kumfungulia Mwanangu moyo wenu safi na mnyenyekevu na hivyo kuweza kupokea vipaji nilivyowaahidi. Hapo ndipo mtakapoongozwa kwa upendo na nguvu za Mwanangu, hapo ndipo mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza kwa walio karibu yao matunda
ya
upendo wa Mungu. Kutokana na ninyi na kwa njia yenu Mwanangu atafanya kazi, maana mtakuwa na Yeye kitu kimoja. Moyo wangu wa kimama unatamani muungano wa wanangu wote, kwa njia
ya
Mwanangu. Kwa upendo mkuu nawabariki na kuwaombea wateule wa Mwanangu, wachungaji wenu, Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Januari 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, salini ili mionzi
ya
sala yenu iwaguse watu wote mnaokutana nao. Wekeni Biblia Takatifu mahali pa kuonekana katika familia zenu, mkaisome ili maneno
ya
amani yatiririke ndani
ya
mioyo yenu. Nasali pamoja nanyi na kwa ajili yenu, wanangu, ili siku hata siku mzidi kuyapokea mapenzi
ya
Mungu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Februari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Kwa upendo wa kimama nataka kuwafundisha uadilifu, natamani kwamba katika kutenda kwenu kazi kama mitume wangu muwe wenye haki, maamuzi na hasa waadilifu. Natamani kwamba, kwa neema
ya
Mungu, muweze kupokea Baraka
ya
Mungu. Natamani, kwa njia
ya
kufunga na kusali, muweze kupata kutoka kwa Baba wa Mbinguni ujuzi, uhalali, utakatifu wa kimungu. Kwa ulinzi wa Mwanangu na wangu mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza neno la Mungu kwa wote wasiolijua, na mtaweza kushinda mapingamizi mtakayokutana nayo njiani. Wanangu, kwa njia
ya
baraka neema itawashukia, nanyi mtaweza kuilinda neema hiyo kwa kufunga na kusali, kwa kujitakasa na kujipatanisha. Mtakuwa na utendaji fanisi ninaohitaji kutoka kwenu. Waombeeni wachungaji wenu ili mionzi
ya
neema
ya
Mungu iangaze njia yao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2014
“
W
anangu wapendwa! Mnaona, mnasikia na kuhisi kwamba katika mioyo
ya
watu wengi hakuna Mungu. Hawamtaki kwa maana wapo mbali na sala na hawana amani mioyoni. Ninyi, wanangu, salini, na isheni kadiri
ya
amri za Mungu. Muwe sala, enyi mlioitikia "naam" tangu mwanzo wa mwaliko wangu. Mshuhudieni Mungu na mtambue uwepo wangu wala msisahau, wanangu,
ya
kuwa mimi ni pamoja nanyi na ninawapenda. Siku hata siku nawachukua kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Naja kwenu kama Mama na ninatamani kuwa kwangu kama Mama mtapata maskani, faraja na mapumziko. Kwa hiyo, wanangu, mitume wa upendo wangu, salini! Salini kwa moyo mkunjufu, utii na uaminifu kamili kwa Baba wa Mbinguni. Muwe na uaminifu, kama vile mimi pia nilivyokuwa mwaminifu nilipoambiwa
ya
kuwa nitachukua baraka za ahadi. Basi kutoka mioyo yenu yafike siku zote midomoni mwenu maneno haya "Utakalo lifanyike". Kwa hiyo muwe na uaminifu na salini, ili mimi niweze kuwaombeeni kwa Bwana, ili awape Baraka
ya
Mbinguni na kuwajaza Roho Mtakatifu. Hapo mtaweza kuwasaidia wale wote wasiomjua Bwana. Ninyi, mitume wa upendo wangu, mtawasaidia kumwita "Baba" kwa uaminifu wote. Salini kwa ajili
ya
wachungaji wenu na mujiaminishe katika mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2014
“
W
anangu wapendwa! Nawaalikeni tena: anzeni kupambana na dhambi kama vile katika siku za mwanzo, nendeni kuungama dhambi zenu na kateni shauri
ya
kuwa watakatifu. Kwa njia yenu upendo wa Mungu utaenea ulimwenguni na amani itatawala mioyoni mwenu na baraka
ya
Mungu itawajaza. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombeeni mbele
ya
Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Next>>