Our Lady of Medjugorje Messages containing 'wa'
Total found:
182
Ujumbe, 25 Aprili 2013
“
W
anangu wapendwa! Salini, salini, mwendelee kusali ili mioyo yenu ifungukie kupokea imani jinsi ua linavyofunguka kuelekea mianga ya joto la jua. Huo ni wakati
wa
neema ambao Mungu anawajalia kwa njia ya uwepo wangu, lakini ninyi mpo mbali na moyo wangu. Kwa hiyo nawaalikeni kwa uongofu binafsi na kwenye sala katika familia zenu. Maandiko matakatifu yawe daima kichocheo chenu. Nawabariki nyote kwa baraka yangu ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Mei 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawaalikeni tena kupenda na kutohukumu. Mwanangu, kwa mapenzi ya Baba aliye mbinguni, alikuwapo pamoja nanyi ili awaonyesheni njia ya wokovu, awaokoeni si awahukumuni. Na ikiwa mnataka kumfuata Mwanangu, msihukumu na mpende, kama vile Baba aliye mbinguni anavyowapenda ninyi. Hata wakati mnapoteseka sana, au mnapojikwaa chini ya msalaba, msikate tamaa, msihukumu, bali kumbukeni kwamba mnapendwa, na msifuni Baba aliye mbinguni kwa upendo wake. Wanangu, msiiache njia ninayowaongozeni. Msikimbie kwenye maangamizi. Kusali na kufunga itawapa nguvu zaidi ili mweze kuishi kama vile baba
wa
Mbinguni atakavyo; ili muwe mitume wangu
wa
imani na upendo; ili maisha yenu iwe na baraka ya wale mnaowaona; ili muwe kitu kimoja na baba aliye mbinguni na Mwanangu. Wanangu, huu ni ukweli
wa
pekee, ukweli uletao wongofu wenu na kisha wongofu
wa
wengine wote wasiojua maana ya neno kupenda. Wanangu, Mwanangu aliwapeni wachungaji: muwalinde, na muwaombee. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 25 Mei 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni kuwa na nguvu na imara katika imani na katika sala, ili sala zenu ziwe zenye nguvu za kuweza hata kufungua moyo
wa
Mwanangu mpendwa Yesu. Salini enyi wanangu wadogo, bila kukoma, ili moyo wenu ujifungue kwa upendo
wa
Mungu. Mimi nipo pamoja nanyi, nawaombea ninyi nyote nikasali kwa ajili ya uwongofu wenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Juni 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, katika wakati huu
wa
wasiwasi nawaalikeni tena kutembea nyuma ya Mwanangu, na kumfuata. Nayajua maumivu, mateso na taabu zenu, lakini katika Mwanangu mtapumzika, ndani yake mtapata amani na wokovu. Wanangu, msisahau ya kuwa Mwanangu amewakomboa ninyi kwa msalaba wake akawajalieni kuwa tena wana
wa
Mungu na kuwafundisha kumwita tena "Baba" yenu, Mungu aliye mbinguni. Ili muwe wapenzi
wa
Mungu Baba, basi muwe na mapendo na msamaha, kwa kuwa Baba yenu ni upendo na msamaha. Salini na fungeni, kwa maana hii ndiyo njia ya kujua na kumfahamu Baba aliye mbinguni. Mtakapomjua huyo Baba, mtafahamu ya kuwa Yeye tu ni muhimu kwenu (Maria Mtakatifu amenena hayo kwa nguvu na amkazo sana). Mimi, nikiwa Mama, nataka wanangu wawe watu wenye umoja ambamo Neno la Mungu husikilizwa na kutekelezwa. Kwa hiyo, enyi wanangu, mfuateni Mwanangu, muwe kitu kimoja naye, muwe wana
wa
Mungu. Pendeni wachungaji wenu kama vile Mwanangu alivyowapenda alipowaita kuwatumikia ninyi. Nawashukuru!
”
Ujumbe, 2 Julai 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo
wa
kimama nawaomba mnipe mioyo yenu ili niweze kumtolea Mwanangu, ili naye aweze kuiokoa, kuiokoa kutoka uovu wote unaowafanya daima kuwa watumwa na unaowafanya kuwa mbali na ule Wema
wa
pekee, yaani Mtoto wangu, anayewaokoa kutoka yote yale yanayowaongoza kwenye njia ya uovu na kuwaondolea amani. Mimi natamani kuwaongoza kwenye uhuru
wa
ahadi za Mtoto wangu, kwa kuwa natamani hapa yatimizwe hasa hasa mapenzi ya Mungu, ili kwa kupatanishwa na Baba
wa
Mbinguni, kufunga na kusali, waweze kuzaliwa mitume
wa
mapendo ya Mungu, yaani mitume watakaoeneza kwa mapendo na uhuru, Mapendo ya Mungu kwa watoto wangu wote, mitume watakaoeneza mapendo aminifu kwa Baba
wa
Mbinguni na hivyo kufungua milango ya mbingu. Watoto wapenzi, toeni furaha ya mapendo yenu na mshikamano wenu kwa wachungaji wenu kama vile Mtoto wangu alivyowaomba wao kutoa furaha hiyo. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Agosti 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, tafadhali muelewe, muwe tayari wote, kwa matumaini makuu, kufungua mioyo yenu; hivyo mngeelewa yote, mngeelewa kwa upendo gani nawaiteni, kwa upendo gani nataka kuwageuza, ili kuwafurahisha, kwa upendo gani nataka kuwafanya wafuasi
wa
Mwanangu na kuwapa amani katika ukamilifu
wa
Mwanangu. Mngeelewa ukuu
wa
moyo wangu
wa
kimama, kwa hiyo, wanangu, salini, maana kwa njia ya kusali tu imani yenu hukua na upendo wenu huzaliwa, upendo ambao utapunguza uzito
wa
msalaba kwa maana hamtakuwa peke yenu kuubeba. Katika umoja na Mwanangu, tukuzeni jina la Baba
wa
Mbinguni. Salini, salini mpate tuzo la upendo, maana upendo ni ukweli
wa
pekee, upendo husamehe yote, hutumikia wote na kuwaona wote kama ndugu. Enyi wanangu, mitume wangu, udhamini ambao Baba
wa
Mbinguni amewawekeni, kwa njia yangu, mtumishi Wake, ni kitu kikubwa, ili kusaidia wale wasiomjua, kusudi zapatanishwe naye, kusudi wamfuate, kwa hiyo nawafundisheni kupenda, maana mkiwa na upendo tu mnaweza kumjibu. Nawaalikeni tena: pendeni wachungaji wenu, salini ili katika wakati huu
wa
shida jina la Mwanangu atukuzwe kwa njia ya mwongozo wao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Agosti 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo pia Yeye Aliye Juu anijalia neema ya kuwa pamoja nanyi na kuwaongoza mpate kutubu. Siku hata siku Mimi napanda mbegu na kuwaalika kutubu ili muweze kuwa sala, amani, upendo na ngano ambayo ikifa huzaa mara mia. Sipendi, wanangu wapendwa, mpate kujuta kwa yote mliyoweza kufanya wala hamkufanya. Kwa hiyo, enyi wanangu, tena kwa moyo
wa
furaha semeni: “ Nataka kuwa ishara kwa watu wengine”. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Septemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, nawapendeni, ninyi nyote, watoto wangu nyote, muwe wote moyoni mwangu, ninyi nyote mmepata upendo wangu
wa
kimama na ninatamani kuwaongoza nyote ili mjue furaha ya Mungu. Kwa hiyo nawaalikeni: nahitaji mitume wanyenyekevu ambao, kwa moyo mkunjufu, wanapokea Neno la Mungu na ambao wako tayari kuwasaidia watu wengine ili, kwa njia ya Neno la Mungu, waelewe maana ya maisha yao. Ili muweze kufanya hayo, wanangu, yawapasa, kwa njia ya kusali na kufunga, kusikiliza kwa moyo mkunjufu na kujifunza kujidhili au kujinyenyekesha. Yawapasa kujifunza kukataa yote yanayowatenganisha na Neno la Mungu na kutamani tu yanayowakaribisha. Msiogope, mimi nipo hapa. Ninyi si peke yenu. Namwomba Roho Mtakatifu ili awafanye wapya, ili awaimarishe. Namwomba Roho Mtakatifu, ili mkisaidia wengine, muweze kujiponya nyinyi wenyewe. Naomba ili, kwa njia yake, muwe wana
wa
Mungu na mitume wangu.
”
Kisha kwa mahangaiko makubwa Bikira Maria alisema:
“
K
wa ajili ya Yesu, kwa ajili ya mwanangu, pendeni wale ambao Yeye aliwaita mkitamani baraka ya mikono ile ambayo Yeye tu ameyaweka wakfu. Msiyaruhusu maovu yatawale. Nawaalikeni tena: ni kwa njia ya wachungaji wangu tu moyo wangu utashinda. Msiyaruhusu maovu yawatenganisheni na wachungaji wenu. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Septemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo pia nawaalikeni kusali. Uhusiano wenu na kusali uwe
wa
kila siku. Sala inasababisha miujiza ndani yenu na kwa njia yenu, na kwa hiyo, enyi wanangu, sala basi iwe ni furaha yenu. Hivyo uhusiano wenu na maisha utakuwa
wa
kina na wazi zaidi, pia mtaelewa kwamba maisha ni zawadi kwa kila mmoja wenu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Oktoba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa! nawapendeni kwa upendo
wa
kimama, na kwa subira ya kimama nangojea upendo wenu na ushirikiano wenu. Nasali ili muwe jumuiya ya wana
wa
Mungu na wanangu. Nasali ili muweze kuwa jumuiya inayojihuisha kwa furaha na imani na upendo
wa
Mwanangu. Wanangu, nawakusanya kama mitume wangu na nitawafundisha jinsi ya kuwajulisha wengine upendo
wa
Mwanangu, na jinsi ya kuwafikishia habari njema, ambaye ni Mwanangu. Nipeni mioyo yenu iliyo wazi na iliyosafishwa, nami nitaijaza upendo
wa
Mwanangu. Upendo wake utaipa maisha yenu maana nami nitatembea pamoja nanyi. Nitakuwa pamoja nanyi hata tumfikie Baba
wa
Mbinguni. Wanangu, wataokoka tu wale ambao watatembea kwa upendo na imani kumwelekea Baba
wa
Mbinguni. Msiogope, nipo pamoja nanyi! Muwaamini wachungaji wenu kama Mwanangu alivyowaamini wakati alipowachagua, na muwaombee ili waweze kupata nguvu na upendo
wa
kuwaongozeni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Oktoba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni mjifungulie kwa sali. Sala itasababisha miujiza ndani yenu na kwa njia yenu. Kwa hiyo, enyi wanangu, kwa moyo mkunjufu mtafuteni Yeye Aliye Juu ili awapeni nguvu ya kuwa wana
wa
Mungu, na yule Shetani asiwatikiseni kama matawi yatikiswavyo na upepo. Kateni shauri tena, wanangu, kwa Mungu na tafuteni tu mapenzi yake, hapo mtapata furaha na amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Novemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa moyo
wa
kimama nawaalikeni tena kupenda, kusali bila kukata tamaa kwa zawadi ya upendo, kumpenda Baba
wa
Mbinguni zaidi ya yote. Mtakapompenda Yeye, mtajipenda wenyewe na jirani zenu. Mambo hayo hayawezi kutengana. Baba
wa
Mbinguni yumo katika kila mtu, hupenda kila mtu na kumwita kila mtu kwa jina lake. Kwa hiyo, wanangu, kwa njia ya kusali sikilizeni atakalo Baba
wa
Mbinguni. Ongeeni na Yeye. Muwe na uhusiano
wa
binafsi pamoja na Baba, atakayeufanya mkubwa zaidi uhusiano wake nanyi, jumuhiya ya wanangu, mitume wangu. Kama Mama napenda kwamba, kwa njia ya upendo kumwelekea Baba
wa
Mbinguni, inukeni juu ya ubatili
wa
malimwengu na muwasaidie wengine kujua na kumjongea polepole Baba
wa
Mbinguni. Wanangu, salini, salini, salini kwa zawadi ya upendo, kwa sababu upendo ndiye Mwanangu. Muwaombee wachungaji wenu, ili wawapende ninyi siku zote, kama vile Mwanangu alivyowapenda ninyi na kuonyesha akitoa maisha yake kwa wokovu wenu. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Leo nawaalikeni nyote kusali. Fungueni kwa kina mlango
wa
mioyo yenu, enyi wanangu, kwa sala, sala ya moyo na hivyo Yeye Aliye Juu ataweza kufanya kazi katika uhuru wenu na kuanzisha uongofu wenu. Hivyo imani yenu itakuwa imara kiasi cha kuweza kusema kwa moyo wenu wote: "Mungu wangu na yote yangu". Halafu mtaweza kuelewa, wanangu, ya kuwa duniani hapa yote hupita. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Desemba 2013 - Mirjana
“
W
anangu wapendwa, kwa upendo
wa
kimama na uvumilivu
wa
kimama naona kutangatanga kwenu na kuendelea kupotea kwenu. Kwa sababu hiyo mimi nipo pamoja nanyi. Nataka kwanza kabisa kuwasaidieni kupata kujijua ninyi wenyewe, ili baadaye muweze kuelewa na kutambua yote yanayowazuia kujua bila unafiki na kwa moyo wote upendo
wa
Baba
wa
Mbinguni. Wanangu, Baba hujulikana kwa njia ya msalaba: kwa hiyo msikatae msalaba: kwa msaada wangu, mkafanye bidii kuuelewa na kuupokea. Mtakapoweza kuupokea msalaba, mtaelewa pia upendo
wa
Baba
wa
Mbinguni. Mtatembea pamoja na Mwanangu na mimi. Mtajipambanua na wale ambao hawakujua upendo
wa
Baba
wa
Mbinguni, kujitofautisha na wale wanaomsikiliza lakini hawamwelewi, na wale wasioenda pamoja naye, na wasiomjua. Mimi nataka ninyi mjue ukweli
wa
Mwanangu na muwe mitume wangu; ili, kama wana
wa
Mungu, muwe na mawazo yaliyo juu ya mawazo ya kibinadamu na siku zote na katika yote mkatafute kila mara mawazo ya Mungu. Wanangu, salini na fungeni ili muweze kuelewa yote ninayowaombeni. Muombee wachungaji wenu mkatamani kujua, mkishirikiana nao, upendo
wa
Baba
wa
Mbinguni. Nawashukuruni.
”
Ujumbe, 25 Desemba 2013
“
W
anangu wapendwa! Ninawaletea Mfalme
wa
amani ili Yeye awapatie amani Yake. Ninyi, wanangu, salini, salini, salini. Matunda ya sala yatajionyesha kwenye nyuso za watu waliojitoa kwa Mungu na Ufalme wake. Mimi pamoja na mwanangu Yesu tunawabariki nyote kwa baraka ya amani. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Januari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Ili mpate kuwa mitume wangu na kuweza kusaidia wale walioko katika giza, ili waweze kuujua mwanga
wa
upendo
wa
Mwanangu, mnapaswa kuwa na moyo safi na mnyenyekevu. Hamwezi kusaidia ili Mwanangu azaliwe na kutawala mioyoni mwa wale wasiomjua, iwapo Yeye hatawali moyoni mwenu. Mimi nipo pamoja nanyi, natembea pamoja nanyi kama mama, nabisha hodi katika moyo wenu, usioweza kufunguka bila ya kuwa mnyenyekevu. Mimi nasali, lakini salini nanyi pia, wanangu wapendwa, ili muweze kumfungulia Mwanangu moyo wenu safi na mnyenyekevu na hivyo kuweza kupokea vipaji nilivyowaahidi. Hapo ndipo mtakapoongozwa kwa upendo na nguvu za Mwanangu, hapo ndipo mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza kwa walio karibu yao matunda ya upendo
wa
Mungu. Kutokana na ninyi na kwa njia yenu Mwanangu atafanya kazi, maana mtakuwa na Yeye kitu kimoja. Moyo wangu
wa
kimama unatamani muungano
wa
wanangu wote, kwa njia ya Mwanangu. Kwa upendo mkuu nawabariki na kuwaombea wateule
wa
Mwanangu, wachungaji wenu, Nawashukuru.
”
Ujumbe, 2 Februari 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Kwa upendo
wa
kimama nataka kuwafundisha uadilifu, natamani kwamba katika kutenda kwenu kazi kama mitume wangu muwe wenye haki, maamuzi na hasa waadilifu. Natamani kwamba, kwa neema ya Mungu, muweze kupokea Baraka ya Mungu. Natamani, kwa njia ya kufunga na kusali, muweze kupata kutoka kwa Baba
wa
Mbinguni ujuzi, uhalali, utakatifu
wa
kimungu. Kwa ulinzi
wa
Mwanangu na wangu mtakuwa mitume wangu, ambao wanaweza kueneza neno la Mungu kwa wote wasiolijua, na mtaweza kushinda mapingamizi mtakayokutana nayo njiani. Wanangu, kwa njia ya baraka neema itawashukia, nanyi mtaweza kuilinda neema hiyo kwa kufunga na kusali, kwa kujitakasa na kujipatanisha. Mtakuwa na utendaji fanisi ninaohitaji kutoka kwenu. Waombeeni wachungaji wenu ili mionzi ya neema ya Mungu iangaze njia yao. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Februari 2014
“
W
anangu wapendwa! Mnaona, mnasikia na kuhisi kwamba katika mioyo ya watu wengi hakuna Mungu. Hawamtaki kwa maana wapo mbali na sala na hawana amani mioyoni. Ninyi, wanangu, salini, na isheni kadiri ya amri za Mungu. Muwe sala, enyi mlioitikia "naam" tangu mwanzo
wa
mwaliko wangu. Mshuhudieni Mungu na mtambue uwepo wangu wala msisahau, wanangu, ya kuwa mimi ni pamoja nanyi na ninawapenda. Siku hata siku nawachukua kwa Mwanangu Yesu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 2 Machi 2014 - Tokeo la Mirjana
“
W
anangu wapendwa! Naja kwenu kama Mama na ninatamani kuwa kwangu kama Mama mtapata maskani, faraja na mapumziko. Kwa hiyo, wanangu, mitume
wa
upendo wangu, salini! Salini kwa moyo mkunjufu, utii na uaminifu kamili kwa Baba
wa
Mbinguni. Muwe na uaminifu, kama vile mimi pia nilivyokuwa mwaminifu nilipoambiwa ya kuwa nitachukua baraka za ahadi. Basi kutoka mioyo yenu yafike siku zote midomoni mwenu maneno haya "Utakalo lifanyike". Kwa hiyo muwe na uaminifu na salini, ili mimi niweze kuwaombeeni kwa Bwana, ili awape Baraka ya Mbinguni na kuwajaza Roho Mtakatifu. Hapo mtaweza kuwasaidia wale wote wasiomjua Bwana. Ninyi, mitume
wa
upendo wangu, mtawasaidia kumwita "Baba" kwa uaminifu wote. Salini kwa ajili ya wachungaji wenu na mujiaminishe katika mikono yao iliyobarikiwa. Nawashukuru.
”
Ujumbe, 25 Machi 2014
“
W
anangu wapendwa! Nawaalikeni tena: anzeni kupambana na dhambi kama vile katika siku za mwanzo, nendeni kuungama dhambi zenu na kateni shauri ya kuwa watakatifu. Kwa njia yenu upendo
wa
Mungu utaenea ulimwenguni na amani itatawala mioyoni mwenu na baraka ya Mungu itawajaza. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombeeni mbele ya Mwanangu. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
Next>>