Our Lady of Medjugorje Messages containing 'nia'
Total found:
2
Ujumbe, 25 Agosti 2014
“
W
anangu wapendwa! Salini kwa
nia
zangu maana Shetani ataka kuangamiza mpango wangu nilio nao hapa na kuwaibia amani: Kwa hiyo, wanangu, salini, salini, salini ili Mungu aweze kutenda kazi kwa njia ya kila mmoja wenu. Mioyo yenu iwe wazi kupokea mapenzi ya Mungu. Mimi nawapendeni na kubariki kwa baraka ya kimama. Asanteni kwa kuitikia mwaliko wangu.
”
Ujumbe, 25 Novemba 2015
“
W
anangu wapendwa, leo ninawaalika nyote: salini kwa ajili ya
nia
zangu. Amani ipo hatarini kwa hiyo wanangu, salini na muwe waletaji wa amani na matumani katika ulimwengu huu wa wasiwasi ambamo shetani anashambulia na kuleta majaribu ya kila aina. Wanangu muwe thabiti katika sala na imara katika imani. Mimi nipo pamoja nanyi na kuwaombea ninyi nyote mbele ya Mwanangu, Yesu. Asanteni kwa kuitikia wito wangu.
”
To compare Medjugorje messages with another language versions choose